Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kikundi hicho cha kigaidi kimewateka watu hao ambao nikatika wahajiri wa Ethiopia, ambapo inasadikiwa kuwa watu hao walikuwa katika gari wakienda mjini Tripoli na kuchukuliwa kupelekwa sehemu isiojulikana.
Msemaji mkuu wa kamati ya kimataifa ya wahajiri wa Ethiopia nchini Libya amethibitisha kutokea kwa tukio, hivyo kwamujibu wa maelezo ya msemaji wa kamati hiyo ni kwamba taarifa ya kutekwa kwa watu hao na kikundi cha kigaidi cha Daesh imetolewa na wahajiri wengine waliokombolewa kutoka mikononi mwa kikundi hicho Jumamosi ya jana.
Mkuu wa kamati pia alisema kikundi cha kigaidi cha Daesh baada ya kuwakamata watu hao walianza kuwauliza maswali ambayo yanahusu masuala ya kiimani ikiwemo jinsi ya sala nk, hivyo wakaweza kuwajua Waislamu na wasiokuwa Waislamu na kuwateka wasiokuwa Waislamu.